Skip to content
  • About Us
  • Disclaimer
  • Telegram Group
Biashara ya Forex

Biashara ya Forex

Forex Trading in Tanzania and Kenya

  • Home
  • Brokers
  • Vitabu vya Forex
  • Help
  • Toggle search form

Forex ni nini?

Posted on January 31, 2019 By Admin No Comments on Forex ni nini?
FOREX ni biashara ya ubadilishaji wa fedha za kigeni ambayo imeonekana kuwa na mzunguko mkubwa zaidi kuliko biashara yoyote dunianini kwani inazungusha zaidi ya dolla za kimarekani trillion 5 kwa siku.

Mtu yoyote anaweza kujifunza biashara ya forex, na kuwa Forex trader mwenye mafanikio. Ili kuwa Forex trader, ni lazima uwe na account ya Forex

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT
Biashara ya Forex imechangiwa sana na mapinduzi ya teknolojia ambapo sasa mtu yeyote unaweza ukafanya biashara hii mahali popoke akiwa na huduma ya mtandao wa intaneti kwa kompyuta au simu janja(smartphone)

  1. Forex ni kifupisho cha FOReign EXchange kwa maana ya biashara ya kununua na kuuza fedha za kigeni. Kama unavyoijua kazi ya Bureau de Change, ndiyo iyo hiyo tunaifanya kwenye Forex sema hii ni ya mtandaoni.
  2. Forex ni biashara halali na inafanyika ulimwenguni mwote na taasisi kubwa kubwa za kifedha na mabenki na central banks.
  3. Biashara hii ni ya mtandaoni na wauzaji na wanunuzi hukutana huko ~soko lake ni la mtandaoni na ni la dunia nzima. Inakadiriwa kuwa, biashara hii imevutia wawekezaji ambao kwa pamoja (wakubwa na wadogo) wanaTRADE zaidi ya US Dollars Trilioni 5.3 kila siku!
  4. Hii biashara kwa kuwa ni ya mtandaoni, ukitaka kuifanya ni lazima uwe na fedha mtandaoni. Unafungua account mtandaoni kama unavyofungua bank, unaweka fedha zako. Unazifanyia biashara na siku ukitaka kuzitoa, unazitoa mtandaoni zinakuwa cash za kutumia.
  5. Biashara hii, kwa kuwa ni ya mtandaoni, unaweza kuifanyia popote! Nyumbani, chumbani, njiani, sokoni..popote! Unahitaji tu vitu vitatu:
    • Computer/Laptop ambayo itakusaidia kuliangalia soko na kujua muelekeo (Market Analysis) 
    • Internet connection. Kwa sababu ni biashara ya mtandaoni, unahitaji kujiung na mtandao.
    • Programu maalum yenye uwezo wa kusoma soko. Hii inaitwa Trading Platform. Hii ni software ambayo, unai~download na kui~install kwenye Computer yako. Hizi ziko nyingi sasa lakn moja maarufu ambayo inatumika sana duniani inaitwa Meter Trader 4 (MT4).

Note 1:
Ni lazima uwe na Computer/Laptop au smartphone na u-install MT4 kama unafanya Market Analysis mwenyewe lkn, kama kuna mtu mwingine anaweza kufanya kwa niaba yako na akakupa kile tunaita Trading Signal, sio lazima uwe na computer, unaweza tu ukawa na simu yako au gadget yoyote ile inayoweza kuunganishwa na mtandao. Note 2:
Baada ya kutimiza hayo, kabla hujaanza KUNUNUA NA KUUZA fedha za kigeni mtandaoni, Ku Trade Forex, unamuhitaji mtukati anayeitwa Broker. Kwanini? Nitafafanua zaidi pale chini lakini, kwa hapa niseme tu, ndiye anayesimama kama bank ya mtandaoni kwako. Utafungua account kwake kama unavyofungua account NMB, NBC, Equity, Exim, n.k. Utampatia taarifa zako zote rasmi, Vitambulisho vyote muhimu, Uraia, Anuani ya unapoishi,…kila kitu. Ndipo atakuruhusu kufungua account ya mtandaoni. Niwaonye wanaopenda kudanganya, hapa usijaribu, utafeli. Hapa wanahitaji taarifa zako halisi na sahihi. Hii ni kwa sababu, hii ni biashara halali kabisa, na ni ya dunia nzima na, inakupatia kipato halali. Sasa, siku umepata faida unataka kuzitoa pesa zako, watakuambia hatukupi maana si wewe, endapo utawasilisha utambulisho mwingine tofauti na ule uliojazaga. Baada ya kuifungua account kwa Broker, unaweka hela zako humo, labda USD, GBP, JPY..utakavyo mwenyewe.

Baada ya hapo, sasa upo tayari kuanza biashara.

Forex ni nini?

Katika kuanza biashara ya Forex, jambo kubwa na la muhimu ni kuhakikisha una trade kupitia broker ambaye yupo regulated, na anaaminika zaidi ili kuepuka matatizo mbali mbali yanayotokana na ku trade kupitia broker asiye na sifa.

Bofya link ifuatayo kutengeneza account kupitia broker anayeheshimika zaidi duniani na mwenye clients zaidi ya 2 milion kutoka nchi mbali mbali duniani ikiwemo Tanzania na Kenya na nchi zote za Afrika Mashariki.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Related Articles

Forex, Forex ni nini, Jifunze Forex

Post navigation

Next Post: Jinsi ya kufanya biashara ya FOREX

Leave a ReplyCancel reply

ZINAZOSOMWA ZAIDI

Maswali na Majibu kuhusu Biashara ya Forex - HelpMay 23, 2022Admin
Jinsi ya kutuma pesa kutoka Safaricom Kenya kwenda Vodacom TanzaniaJinsi ya kutuma pesa kutoka Safaricom Kenya kwenda Vodacom TanzaniaJanuary 7, 2020Admin
Broker wa Forex anayeruhusu kuweka na kutoa pesa kupitia mitandao ya simuBroker wa Forex anayeruhusu kuweka na kutoa pesa kupitia mitandao ya simuNovember 29, 2021Admin

MAKALA MPYA

  • Broker wa Forex anayeruhusu kuweka na kutoa pesa kupitia mitandao ya simu
  • Jinsi ya kuchagua broker mzuri wa Forex
  • Jinsi ya ku trade Volatility Index kwa kutumia Binary
  • Jinsi ya kutuma pesa kutoka Safaricom Kenya kwenda Vodacom Tanzania
  • Jinsi ya kudeposit Templerfx kwa kutumia Safaricom M-Pesa
Copyright © 2022 - All Rights Reserved