Skip to content
Biashara ya Forex

BIASHARA YA FOREX

Forex Trading in Tanzania and Kenya

  • Home
  • Brokers
  • Mobile App
  • Vitabu vya Forex
  • Help
  • Contact Us
  • Toggle search form

Jinsi ya ku-verify account yako ya Templerfx (Full Verification)

Posted on June 19, 2019May 17, 2022 By Admin No Comments on Jinsi ya ku-verify account yako ya Templerfx (Full Verification)

Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema na safari yako ya mafanikio kupitia biashara ya Forex.

Jinsi ya kuverify account ya forex

Leo tutaenda kuangalia ni namna gani ya kuweza kupata full verification templerfx account, ambayo itakuwezesha kufanya mambo mbali mbali kwa uwepesi ikiwepo kuwa na njia nyingi zaidi za ku deposit na ku withdraw pamoja na kuwa na uwezo wa kuomba salio la bure la dola 30 za kuanzia ku trade Forex (No Deposit Bonus)

Ikiwa umeshatengeneza account yako ya Forex, utaona kwamba unatakiwa ufanye verification (uthibitisho) katika maeneo makuu matano, na iwapo bado huna account ya Forex, basi bonyeza kutufe kifuatacho kutengeneza account hiyo bure kabisa:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Kama tayari una account ambayo haijawa verified, utatakiwa kufanya verification ya:

  1. Email Address
  2. Namba yako ya simu
  3. Kitambulisho chako (Identity Verification)
  4. Address Vefirication (Uthibitisho wa makazi) 
  5. Credit Card Verification (Uthibitisho wa kadi yako ya bank)

Ukishatengeneza account yako ya templerfx, utapaswa ku login kwenye account yako na kwenda kwenye menu, kisha bofya sehemu iliyoandikwa My TemplerFx na kwa chini yake utaona sehemu imeandikwa Verification, bofya sehemu hiyo, na fuata maelekezo kwa vipengele vyote vitano, ingawa vipengele muhimu ni vitatu, yaani Email, Namba ya simu na Identity verification.

Jinsi ya kuverify

1. Kuthibitisha Barua pepe (email)

Hii itakupasa kwenda kwenye inbox yako ya Email, na utabofya link utakayotumiwa ku-confirm email address yako.

2. Kuthibitisha Namba yako ya simu

Hi itakupasa kubofya kitufe cha ku verify namba yako ya simu, halafu automatically utatumiwa SMS yenye namba ya uthibitisho, nakili namba hiyo halafu iandike kwenye kibox utakachoulizwa, baadae bofya confirm, na namba yako itakuwa imeshathibitishwa na utaona tick la kijani.

3. Kuthibitisha Kitambulisho chako.

Kuthibitisha kitambulisho chako (Identity Verification) utapaswa kupiga picha kitambulisho chako kinachokubalika kwa mfano Leseni ya Udereva, kitambulisho cha mpiga kura, passport au kitambulisho cha uraia. Halafu utaki-upload kitambulisho hicho kwa ku bofya sehemu iliyoandikwa “Upload Identity” itakuchukua masaa kadhaa kuthibitishwa, na ukishathibitishwa utaona tick ya kijani kwamba umeshathibitishwa.

4. Kuthibitisha Anuani ya Makazi.

Kuthibitisha anuani ya makazi ni jambo muhimu kwenye biashara ya forex, na ni sehemu ya kitu kinachoitwa KYC au Know Your Customer. Njia rahisi ya kuthibitisha anuani ya makazi, ni kwenda kuomba statement ya account yako ya bank hata ya muda mfupi, hakikisha statement hiyo ina jina lako kamili na anuani yako, halafu utai upload statement hiyo na baadae account yako itapata address verification ambapo utaona umewekewa tick ya kijani.

5. Kuthibitisha kadi ya bank

Mwisho kabisa utatakiwa kuthibitisha kadi yako ya bank, hii ni muhimu pale unapotaka kuomba dola 30, za kuanza ku trade Forex (No Deposit Bonus) na pia ni muhimu pale unapotaka ku deposit kwa kutumia njia ya SKRILL

Ukifanikiwa kufuata vipengele vyote vya uthibitisho wa account yako kama nilivyoeleza hapo juu, utakuwa umefanikiwa kuwa na FULL VERIFIED templerfx account ambayo itakuwezesha ku trade forex na kutumia huduma zote zinazotolewa na broker wako.

Iwapo huna account ya Forex hadi sasa, usisite kuanza kwa kusoma post hii inayoelezea jinsi ya kujiunga na forex:

Jinsi ya kujiunga na biashara ya Forex

Na iwapo ungependa kufungua account ya Forex, bofya kitufe kifuatacho:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Endelea kuwa pamoja nami katika kujifunza mbinu mbali mbali za mafanikio kupitia Forex

Related

Bonus, TemplerFx, Verification

Post navigation

Previous Post: Mbinu kuzuia hasara kwenye biashara ya Forex
Next Post: Namna ya kufanya biashara ya Forex

Leave a Reply Cancel reply

Archives

  • November 2021
  • April 2020
  • February 2020
  • January 2020
  • October 2019
  • September 2019
  • July 2019
  • June 2019
  • May 2019
  • February 2019
  • January 2019

Categories

  • AirTel Money
  • Beginner
  • Best Forex Brokers in Kenya
  • Best Forex Brokers in Tanzania
  • Biashara ya Forex
  • Binary Options
  • Bonus
  • Brokers
  • Capital
  • Demo
  • Demo Account
  • Deposit
  • Education
  • Exness
  • Exness Tanzania
  • Forex
  • Forex kwa kiswahili
  • Forex ni nini
  • Forex Regulators
  • Free 30 USD
  • Jifunze Forex
  • Kenya
  • M-Pesa
  • M-Pesa Kenya
  • Mastercard
  • Meta Trader 4
  • Meta Trader 5
  • No Deposit Bonus
  • Real Account
  • Regulated Brokers
  • Risk Management
  • Safaricom
  • Safaricom M-Pesa
  • Skrill
  • Skrill Tanzania
  • Support and Resistance
  • Tanzania
  • Technical Analysis
  • TemplerFx
  • TickMill
  • TigoPesa
  • Verification
  • Visa
  • Vodacom M-Pesa
  • Volatility Index

Recent Posts

  • Broker wa Forex anayeruhusu kuweka na kutoa kupitia mitandao ya simu kama Mpesa na tigopesa
  • Jinsi ya kuchagua broker mzuri wa Forex
  • Jinsi ya ku trade Volatility Index kwa kutumia Binary
  • Jinsi ya kutuma pesa kutoka Safaricom Kenya kwenda Vodacom Tanzania
  • Jinsi ya kudeposit Templerfx kwa kutumia Safaricom M-Pesa

Recent Comments

No comments to show.
Copyright © 2022 - All Rights Reserved