Skip to content
  • About Us
  • Disclaimer
  • Telegram Group
Biashara ya Forex

Biashara ya Forex

Forex Trading in Tanzania and Kenya

  • Home
  • Brokers
  • Vitabu vya Forex
  • Help
  • Toggle search form

Mbinu kuzuia hasara kwenye biashara ya Forex

Posted on June 11, 2019April 20, 2024 By Admin No Comments on Mbinu kuzuia hasara kwenye biashara ya Forex

Iwapo ndio kwanza umeanza biashara ya Forex, au tayari ni trader mzoefu wa Forex, jambo la msingi kabisa ambalo unapaswa kuzingatia muda wote unapofanya biashara hii ni namna ya kuhakikisha kwamba pesa yako inabaki salama kwa kuzingatia mbinu mbali mbali zenye lengo la kuhakikisha unaepukana na uwezekano wa kuunguza account yako au kufunga positions zako kwa hasara kubwa.

Forex Risk Management

Zipo mbinu mbali mbali ambazo trader unapaswa kuzizingatia ili kuweza kuwa na uhakika wa pesa yako kubaki salama.

Iwapo ndio unaanza kujifunza Forex, na bado hujatengeneza account, bofya kitude kifuatacho kujiunga na Forex:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Kama tulivyokwisha kusoma kwenye post zilizopita pamoja na angalizo juu ya biashara ya Forex, unapaswa kufahamu kwamba haijalishi kwamba una uzoefu na elimu kiwango gani juu ya Forex, muda wowote unaweza kupata hasara itakayopelekea sehemu au pesa yako yote kupotea.

Sasa ili angalau kuweza kuzuia hasara au upotevu wa pesa yako kwenye biashara hii ya Forex, yakupasa kuzingatia mambo yafuatayo:

1. Soma na Fuatilia

Kujifunza kuhusu Forex, jinsi inavyofanya kazi, misingi yake na technique zake zote ndio msingi mkubwa wa mafanikio katika biashara ya Forex. Iwapo utaamua kuwa Forex trader, basi yakupasa uwe makini na kuwa active kwenye kufuatilia mambo mbali mbali au news zinazoweza kupelekea movement kubwa kwenye masoko ya Forex, jambo hili litakusaidia kufanya maamuzi sahihi pale unapoamua kuingia sokoni.

Kusoma na kufuatilia, kutakufanya kuwa na hali ya kujiamini pale unapoamua kuingia sokoni kwa kuwa yapo matukio makubwa ya kisiasa na kiuchumi yanayoweza kugeuza uelekeo wa soko ghafla na kujikuta ukiingia kwenye hasara kubwa.

2. Epuka Brokers wanaolalamikiwa sana

Uzuri tunaishi kwenye nyakati ambazo ni rahisi kufahamu heshima/reputation ya broker unayetaka kujiunga naye, waweza kufahamu zaini kuhusu broker huyo kwa ku search kwenye mtandao au kutembelea tovuti iitwayo ForexPeaceArmy ili kufahamu ni kiwango gani cha malalamiko broker huyo anayo, ni vizuri pia kufahamu mambo mbali mbali kuhusu broker huyo ikiwa ni pamoja na kufahamu njia za kuweka na kutoa pesa, ufahamu fee zao, na pia hakikisha ni broker ambaye yupo regurated na vyombo vinavyoheshimika kufanya regulations za taasisi za fedha.

3. Anza na account ya majaribio (demo account)

Tumeshajifunza jinsi ya kutengeneza account ya demo kwa ajili ya kuanza ku practise ku trade Forex, waweza soma post hii:

Jinsi ya kufungua na kutumia Demo account kwenye Forex

Ni vyema kabla hujaanza kuweka pesa zako kwenye Forex, ukajaribu kutumia demo account ili kujifunza zaidi na kupima uelewa wako juu ya ku trade Forex, vinginevyo kama huna ufahamu wa kutosha, ukikimbilia kuanza ku trade moja kwa moja kwa real account, utapoteza fedha zako.

4. Epuka kutumia Leverage kubwa sana

Moja kati ya sababu zinazofanya Forex ipendwe zaidi ni matumizi ya leverage, leverage ni utaratibu unaowekwa na broker wa kuhakikisha kwamba una uweza wa kupata faida kubwa hata kama kiwango chako ulicho deposit ni kidogo, leverage ni uwiano wa kiwango cha pesa ulicho nacho, na kiwango cha pesa unacho trade. Matumizi ya leverage kubwa yanakupa uwezekano wa either faida kubwa sana, au hasara kubwa sana kwa muda mfupi.

Related Articles

Beginner, Forex, Risk Management

Post navigation

Previous Post: Jinsi ya kucheza forex
Next Post: Jinsi ya ku-verify account yako ya Templerfx (Full Verification)

Leave a ReplyCancel reply

ZINAZOSOMWA ZAIDI

Jinsi ya kutuma pesa kutoka Safaricom Kenya kwenda Vodacom TanzaniaJinsi ya kutuma pesa kutoka Safaricom Kenya kwenda Vodacom TanzaniaJanuary 7, 2020Admin
Jinsi ya kuchagua broker mzuri wa ForexJinsi ya kuchagua broker mzuri wa ForexApril 6, 2020Admin
Broker wa Forex anayeruhusu kuweka na kutoa pesa kupitia mitandao ya simuBroker wa Forex anayeruhusu kuweka na kutoa pesa kupitia mitandao ya simuNovember 29, 2021Admin

MAKALA MPYA

  • Broker wa Forex anayeruhusu kuweka na kutoa pesa kupitia mitandao ya simu
  • Jinsi ya kuchagua broker mzuri wa Forex
  • Jinsi ya ku trade Volatility Index kwa kutumia Binary
  • Jinsi ya kutuma pesa kutoka Safaricom Kenya kwenda Vodacom Tanzania
  • Jinsi ya kudeposit Templerfx kwa kutumia Safaricom M-Pesa
Copyright © 2022 - All Rights Reserved