Skip to content
Biashara ya Forex

BIASHARA YA FOREX

Forex Trading in Tanzania and Kenya

  • Home
  • Brokers
  • Mobile App
  • Vitabu vya Forex
  • Help
  • Contact Us
  • Toggle search form

Jinsi ya kutumia Metatrader 4 mt4 ku trade Forex

Posted on June 24, 2019May 17, 2022 By Admin No Comments on Jinsi ya kutumia Metatrader 4 mt4 ku trade Forex

Makala hii itaenda kukuelimisha jinsi ya kutumia program ya Metatrader 4 au kwa kifupi mt4 kukuwezesha kufanya biashara ya Forex.

Jinsi ya kutumia Metatrader 4 mt4 ku trade Forex

Metatrader ni program maalum inayotumika kuwezesha ufanyaji wa biashara ya Forex yaani kufungua position, pamoja na kukupatia chart ambazo zitakuwezesha kuona uelekeo au historia ya pair za Forex na pia kukuwezesha kufanya uchambuzi wa pair hizo kwa kitaalam technical analysis.

Kuanza kutumia program hii, yakupasa uwe na account katika moja ya broker utakayemtumia ku trade Forex.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Metatrader ina version kuu mbili, Metatrader 4 na Metatrader 5, hizi ni programu mbili tofauti na haimaanishi kwamba Metatrader 5 ni toleo la juu la metatrader 4, la hasha. Hizi ni program tofauti kabisa, ingawa zinatengenezwa na kampuni moja, na programu ambayo inatumika zaidi kwa biashara ya Forex, ni Metatrader 4 au kwa kifupi MT4.

Jinsi ya ku-install Metatrader4

Program ya Metatrader 4 inapatikana katika vifaa vyote tunavyotumia ku trade Forex yaani simu, PC pamoja na Mac. Zipo version za mt4 za Android, iOS na hata Windows kwa ajili ya computer yako.

Kuweza kutumia vyema program hii ya Metatrader 4, yakupasa uwe umeshafungua account kwa broker unayemtumia.

Ukishatengeneza account, aidha kwa kutumia simu yako ya mkononi au kwa kutumia computer yako, fungua menu, au angalia menu iliyopo upande wa kushoto, utaona menu imeandikwa Downloads, bofya sehemu hiyo kisha bofya sehemu iliyoandikwa Platforms na utaona maelekezo pamoja na orodha za platform ambazo unatumia ili u download program hii ya Metatrader 4. Kama unatumia windows computer, bofya sehemu iliyoandikwa  TemplerFX trader on windows, na kama unatumia simu ya mkononi, nenda moja kwa moja kwenye PlayStore kama unatumia Android, au AppStore kama unatumia iPhone au iPad, kisha search neno MT4 au neno Metatrader4 ambapo utaona program hii, na utai install.

Ukisha install, utaona option ya kufungua Demo account, ambapo una uhuru wa kufungua default demo account kutoka kwa watengenezaji wa program ya mt4, au waweza ingiza taarifa za demo account za broker wako.

Kama hutapenda kuweka demo account, una uhuru wa kuweka login na password zako za account yako uliyotengeneza kwa broker wako.

Kumbuka kwamba, taarifa zako za ku login, zipo kwenye site ya broker wako, kama unatumia broker wa templerfx, basi kupata taarifa zote, login kwenye site ya templerfx, halafu kwenye menu kuu, bofya sehemu iliyoandikwa Open an Account halafu chini yake, bofya new account.  Kwenye orodha ya account za kutengeneza, utaulizwa uchague aina ya account ya kutengeneza, chagua yoyote inayokufaa kati ya either DEMO ACCOUNT (kama hupo tayari kuanza na real account) au chagua LIVE UNIVERSAL FX kutengeneza live/real forex account.

Jinsi ta kufungua account ya mt4

Mara baada ya kutengeneza, utapewa Login Id, na Password. Ambazo sasa, ndio unazopaswa kuzitumia ku login kwenye program yako ya Metatrader 4.

Endelea kuwa nasi katika makala hii ambayo itaendelea kukufundisha jinsi ya kutumia menu mbali mbali zilizopo kwenye program uliyo install ya Metatrader 4.

Napenda kukufahamisha tena, kama huna account bado, bofya link ifuatayo kutengeneza account yako ya Forex.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Kama una maoni, ushauri, au swali, usiache kutushirikisha kwa kuandika kwenye sehemu ya comments, au kuwasiliana nasi kwa kubofya menu ya Telegram hapo juu.

Related

Demo Account, Meta Trader 4, Real Account

Post navigation

Previous Post: Namna ya kufanya biashara ya Forex
Next Post: Jifunze Forex: Jinsi ya kutambua supply and demand zones

Leave a Reply Cancel reply

Archives

  • November 2021
  • April 2020
  • February 2020
  • January 2020
  • October 2019
  • September 2019
  • July 2019
  • June 2019
  • May 2019
  • February 2019
  • January 2019

Categories

  • AirTel Money
  • Beginner
  • Best Forex Brokers in Kenya
  • Best Forex Brokers in Tanzania
  • Biashara ya Forex
  • Binary Options
  • Bonus
  • Brokers
  • Capital
  • Demo
  • Demo Account
  • Deposit
  • Education
  • Exness
  • Exness Tanzania
  • Forex
  • Forex kwa kiswahili
  • Forex ni nini
  • Forex Regulators
  • Free 30 USD
  • Jifunze Forex
  • Kenya
  • M-Pesa
  • M-Pesa Kenya
  • Mastercard
  • Meta Trader 4
  • Meta Trader 5
  • No Deposit Bonus
  • Real Account
  • Regulated Brokers
  • Risk Management
  • Safaricom
  • Safaricom M-Pesa
  • Skrill
  • Skrill Tanzania
  • Support and Resistance
  • Tanzania
  • Technical Analysis
  • TemplerFx
  • TickMill
  • TigoPesa
  • Verification
  • Visa
  • Vodacom M-Pesa
  • Volatility Index

Recent Posts

  • Broker wa Forex anayeruhusu kuweka na kutoa kupitia mitandao ya simu kama Mpesa na tigopesa
  • Jinsi ya kuchagua broker mzuri wa Forex
  • Jinsi ya ku trade Volatility Index kwa kutumia Binary
  • Jinsi ya kutuma pesa kutoka Safaricom Kenya kwenda Vodacom Tanzania
  • Jinsi ya kudeposit Templerfx kwa kutumia Safaricom M-Pesa

Recent Comments

No comments to show.
Copyright © 2022 - All Rights Reserved