Jifunze Forex: Jinsi ya kutambua supply and demand zones

Supply na demand hizi ni kanda au zone ambazo zinapatikana katika chart ya forex, hizi zone huwa ndio zinazozingatiwa sana na matrader wote wa aina tatu, ambao ni seller buyer na institutions, ambao seller na buyer kwa neno moja tunawaita retailer yani wafanya biashara wadogo wadogo na hao walio kwenye taasisi mbali mbali ambazo zinajihusisha katika biashara hii ndio hao tunawaida wafanya biashara wakubwa na ndio hasa wenye nguvu katika soko hili la forex.

N.B:

Kama ndio unaanza kujifunza biashara ya Forex, unashauriwa kujiunga kwa kutengeneza account kwa broker anayekubalika zaidi Afrika Mashariki:

Ukishatengeneza account yako ya Forex, usisahau ku verify email uliyotumia kutengeneza account pamoja na namba yako ya simu

Tuendelee na somo letu la leo:

Jifunze Forex Kiswahili

Kwa hiyo kwakua wafanya biashara wote huwa wanaheshimu zones(ukanda) basi hii inapelekea uhakika zaidi pindi unapotrade kwakutumia zone, maana ndipo jicho la kila mfanya biashara lilipo duniani kote.

Kama nilivyosema hapo juu kwamba support na resistance huwa hazina utofauti sana na supply na demand kwa kuziangalia kwa macho ila kiufundi huwa utofauti upo tena ni wamuhimu sana na ili utrade hii strategy ni lazima uzingatie utofauti huo, maana usipozingatia huo utofauti utakua umetoka kwenye maana halisi ya supply na demand na unaingia kwenye support na resistance

Utofauti uliopo kati ya demand na supply ukilinganisha na support na resistance ni kwamba support na resistance huwa yenyewe inasisitiza sana kwenye idadi ya candlestick ambazo zinagusa kwenye hizo mistari ya support na resistance huwa kadri inavyogusa Mara nyingi na kushindwa kuvuka upande wa pili wa huo mstari basi ndio uimara wa huo mstari wa support au resistance unavyoongezeka.

Ila kwenye supply na demand hii kitu imekataliwa kabisa na kuna sababu nyingi ambazo zimetolewa zinazofanya hiyo point ikataliwe, huku wanasema kwamba ili zone ya demand au supply iwe imara basi ni lazima iguswe na candle moja mbaka tatu zikizidi hapo basi hiyo si ukanda imara kwahiyo achana nao, sasa wakatoa sababu za kwanini haiwi zone imara ikiguswa na candle ya zaidi ya mbili au tatu…tutaziona hapo chini

Kumbuka haya masomo yote nnayoyatoa hapa ni elimu so ni muhimu na wewe ukapita pita kwenye vitabu ili upate zaidi…nnavyosema elimu namaanisha ni kitu nlichobaki nacho kichwani baada ya kupita pita kwenye vitabu vingi so nenda kaongeze maarifa kwenye vitabu baada ya hapa ili upate mengi ambayo hayapo kwenye elimu yangu ndogo, nikiwa na maana kwamba nimeyasahau.

Sababu ya kwanza ya kwanini supply na demand strategy imekataa kwamba idadi ya miguso mingi kwenye ukanda si uimara wa ukanda huo.

Kwanza tupate picha then tutaenda kwenye sababu moja kwa moja, kama tulivyowahi kusema huko juu kwamba soko huwa linamove up and down na wakati mwingine linakua limekaa kwenye usawa na likiwa linapanda juu huwa tunasema demand wananguvu kuliko supply na likiwa linashuka chini huwa tunasema supply wananguvu kuliko demand na likiwa katika usawa hapa tunasema supply na demand wote wako na nguvu sawa.

Kwahiyo ili soko litembee kwenda juu au kurudi chini ni lazima kuwe na kuzidiana kwa nguvu kati ya demand na supply na endapo wakitoshana nguvu basi soko huwa linakua linafanya haki, yani watakao nunua watanunua sawa na watakao uza.

Kwahiyo kutokana na sababu hii ya kinachopelekea soko litembee juu chini au chini juu, ndio sababu ya kwanza inayopelekea supply na demand kukataa ile dhana ya kwamba eti uimara wa zone unapimwa na idadi ya miguso mingi ya candlestick.

Kwa sababu endapo ukanda utaguswa na candle Mara nyingi hii inamaanisha supply na demand nguvu zao hazina utofauti sana au ndio zinaelekea kwenye uwiano sawa, ila endapo itaguswa na candle moja au mbili then reaction ya kwenda juu au chini ikawa imetokea basi hapo tunasema demand na supply hawako katika usawa na hapo lazima kutakua na pips nyingi sana.

Pia kama hujaelewa hapo njoo kwenye mfano huu mwingine wa kawaida sana tu.

Kwamfano chukua kitenesi kidundishe kwenye sakafu then kiangalie vile kitakwenda juu na kurudi kugonga sakafu then kitakwenda baadae kitapungua kasi na baadae zaidi kitaishiwa nguvu na kitaanza kuroll na hatimae kitatulia sehemu moja…basi hata kwenye zone candlestick zitakwenda zitagusa na kugusa tena na tena na baadae zitatulia hapo kwa muda mwingi bila kushuka sana wala kwenda upande wa pili, so kadri zone inavyoguswa Mara nyingi ndio udhaifu wake unaongezeka…..kwenye mpira ukiruhusu timu pinzani iwe inakuja kwenye himaya yako Mara kwa Mara lazima utafanya makosa tu na utaachia na utafungwa goal so miguso ikitokea mingi itafikia mahali usawa utaonekana na usawa ukitokea basi ukatili utafuata(initiative), hii ndio tofauti ya hao jamaa na ndio maana kuna watu wanasemaga support na resistance haina jipya nlimskiaga mtu aliwahi sema hivi pia na marumbano yalikua mengi mno ingawa sijajua kama na yeye alitumia point hii au alikua na maana nyingine.

Kwa kawaida head and shoulder pattern huwa inakua na mabega mawili la upande wa kushoto na upande wa kulia na katikati ya mabega hayo huwa kuna head.

Kimsingi ili head and shoulder iwe valid kwa kiasi kikubwa ni lazima bega la upande wa kushoto liwe kubwa kuliko la upande wa kulia, ndio ikiwa hivi hapa tunakua na uhakika zaidi kuliko kinyume chake….najua utauliza kwanini sasa iwe hivi?, inakua hivi kwasababu zifuatazo.

Kwa kawaida head and shoulder ili itokee ni lazima kuwa na strong momentum ama kwenye support au resistance na hiyo strong momentum inapelekea support au resistance ivunjwe na price itaenda juu bila kufanya pullback baada ya kuvunja support au resistance itaenda juu kwa umbali flani then itakutana na demand au supply wengi so hao waliofanya hiyo initiative wataingiwa na wasiwasi wataanza kuchukua partial profit na kitendo cha kufanya hivi basi itapelekea retracement kutokea na hii retracement itakua kipimo cha kwanza kwa hao waliofanya initiative wataitumia hii kupima nguvu zao, sasa wataitumiaje kupima nguvu zao, twende tuone huu mfano hapa chini.

Majeshi ya nchi Fulani yanapotaka kuvamia nchi nyingine kwa kawaida huwa mashambulizi yanaanzia kwenye mpaka, so wataweka ngome mpakani then wataanzia hapo kuingia ndani ya hiyo nchi kwa mashambulio ya taratibu, ila pia kuna ile unaingia kwa nguvu zote ili kuwaogopesha zaidi then ukiona nao wamejipanga zaidi unarudi nyuma kuweka ngome kwenye mipaka yao ili watakapokuja wewe uanze kuwashambulia hapo, basi ndivyo ilivyo baada ya kuvunja let say support hawakusubiri pullback wakaingia wakakuta nguvu zao nyingi ila hazina effect kubwa so wanaamua kurudi nyuma kwenye zone wanaweka pending order nyingi hapo na hao wa upande wa pili wakifika hapo wanakua hawana uwezo wa kupita upande wa pili na hapo demand wataichukua hiyo nafasi na kuipeleka price juu kwa kasi coz wataona hao jamaa kumbe ni dhaifu maana wameweza kuwaingilia kwenye ukanda wao kwa kasi ila wao wameshindwa kutumia nguvu nyingi kurudisha hayo mashambulizi na kiwarudisha hao demand kwenye zone yao ila wanaishia kwenye mpaka ambao ndio support na hii ndio itawafanya jamaa waongeze nguvu nyingi na kuipeleka price juu zaidi na hapa ndio tunatengeneza head wakati huo bega la kushoto ndio limetengenezwa kwa ile initiative na retracement iliyofanyika so ikishaenda juu itafika kwenye zone ambayo hao jamaa nao wako wengi na pia majeshi ya upande wa pili yataingiwa na hofu so wataanza kupunguza kasi na hapo demand wataanza kuchukua profit zao na kitendo hiko kitapelekea supply waongeze nguvu na kurudisha price chini tena na price ikifika kwenye mpaka yani support itakutana na jamaa bado wapo wengi sana hapo wanasubiri mguso wa pili uje waende nao juu lakini kumbuka wakati initiative inatokea kutengeneza bega la kushoto supply walikua hawakujipanga so baada ya kuona hiyo initiative basi nao wataweka pending order zao mwisho wa hilo bega kwahiyo baada ya mguso wa pili wa kukamilisha head kwenye support, demand watachukua price kwenda juu lakini wakati huo supply wamesogeza ngome karibu yani pale ambapo bega la kushoto limeishia ili wakirudi tena hao demand wasiende mbali zaidi so demand wakifika eneo hilo wanakutana na supply wengi sana na hapo watashindwa kwenda mbali zaidi na price itarudishwa chini tena hapo bega la kulia linakua limekamilika so head and shoulder inakua imekamilika.

Je head and shoulder ni lazima ishuke chini endapo itakua kwenye support? Jibu ni hapana, coz forex si science ila kinachopeleka price up and down ni hali ya utofauti wa uwiano kati ya demand na supply na alama inayotuonesha kwamba supply ana nguvu kuliko demand au kinyume chake basi ni uwezo wa kuipeleka price kwenye zone ya mwenzie bila vikwazo au kuonesha vikwazo wakati unapotaka kushamuliwa kwenye ngome yako.

So kwenye head and shoulder shambulio la bega la kwanza ni lakushtukiza na baadae ikapelekea head na baada ya hapo hao watu wa upande wa pili wataona ela zao nyingi zinapotea au currency yao inakua weak so ili kuipandisha ni lazima waongeze nguvu wauze sana na hapo watakamilisha kichwa na wakifika kwenye zone tena

hawaendi kwa papara watajipanga upya ili kujua nguvu iliyopo upande wa pili kama bado ni ile ile au inapungua na ili wagundue hilo watasogeza zone usawa wa bega la kwanza na hao demand wakishindwa kupita hapo basi watajua kweli wamelegea so wataongeza nguvu zaidi na hatimae kuishuka price chini kwa kuingia kwenye zone yao na hii huwa inatokea sana kulingana na session husika na currency zilizounda pair husika zinauhusiano gani na hiyo session..

Na nlisema patten ni lazima zianze kwenye zone au ziishie kwenye zone, sasa hii pattern ya head and shoulder huwa inatokea kwenye zone na inaishia kwenye zone ila mabega yake huwa yanatengeneza minor zone, but kichwa huwa kinakua kwenye major zone na huku chini tunakoweka neckline huwa ni kwenye major zone pia

Jifunze Forex Kiswahili

 Huu ndio mfano wa head and shoulder
Ukiangalia hiyo picha utagundua imetokea kwenye support na maelezo yote nliyoyatoa hapo juu yako hapo kwenye picha, ila hapa nataka nielezee kwanza kwa kuunganisha na concept ya supply na demand.

Angalia hapo sasa kwenye neckline utaona hiyo zone imeguswa zaidi ya Mara moja na kama tunavyosema zone kadri inavyoguswa Mara nyingi ndivyo inavyopoteza ubora so baada ya kupoteza ubora nadhani umeona kilichofuta….hii ni confluence ya kwanza.

Pia confluence ya pili ni kwamba ukiangalia upande wa kulia wa hiyo head na bega hilo la kulia utagundua price imeform flat pattern ambayo hii inaonesha kwamba trend imeshabadilika si up tena ila ni down.

Why down ni kutokana na formation higher high ambayo ndio hiyo head then baada ya hapo ikashuka kuform lower high na lower low.

So hapo ndio tunapata confluence ya pili kwamba kuna uwezekano mkubwa wa hiyo price kushuka chini but hii sio sheria ila ni lazima tujue balance ya supply na demand ndio hasa inayosababisha market I move
Technical analysis inatusaidia kutambua mipaka iliyopo kati ya supply na demand ila si kwamba ndio hasa inapeleka soko juu na chini, so si kila mchoro unaouchora na ukausoma ukataka ufanye kazi kama vile ulivyosoma hapo utakua unaifanya forex iwe science wakati haiko hivyo
Nlisema hizi pattern kuna wakati huwa zinaathiriwa sana na session flani flani hasa hizi za triangle ila hizi za divergence Mara nyingi huwa zinatokea wakati soko linapokua haliko kwenye trend yani soko linapofanya fair treatment(haki), so huwa inapoonekana tu lazima ifuate uelekeo wake kwa asilimia kubwa ingawa sio sana, unaweza ukachunguza hii

Soko linapokua kwenye pattern hasa za triangle watu huwa wanafananishaga na mnada,  ndio mnada…kwamba kwenye mnada huwa kunakuaga na mtajo wa bei kutoka chini kwenda juu yani bei inapanda kuzidiana so mwenye ela nyingi anampiku mwenzie so kuna wale ambao huwa wanasubiri hadi bei inapogota sehemu Fulani na ikawa hakuna yeyote ambae anauwezo wa kuongeza juu so hapo ndio anagundua kwamba wameshindwa hawana uwezo tena wa kifedha so yeye ni muda wake wa kuongeza ela kuchukua hiyo bidhaa….Basi ndivyo ilivyo kwa forex tunapokua katika pattern let say ya triangle labda katika pair ya EURUSD katika session ya Asia na hiyo pattern ikadumu hadi asubuhi muda wa London basi hapo kuna uwezekano mkubwa mabadiliko yakatokea na mabadiliko hayo yatambeba zaidi EUR kwa maana hiyo session ya London ndio moja ya currency ambazo zinakipaombele sana pamoja na GBP….ila ikatokea kuanzia asubuhi London imefunguliwa hadi mida ya kukaribia New York session hakuna mabadiliko yoyote kwenye ile pattern basi hapo lazima dollar atakua na uwezo mkubwa wa kufanya initiative coz wataona jamaa wameishiwa nguvu so wao wakiingiza nguvu mpya basi lazima waendeshe price iwe upande wao, but kama nao watashindwa basi choppy itaendelea kuendelea so ndio maana nkasema kama mnada coz kuna mtegeano wa nyakati kabla ya kufanya maamuzi.

Kuna kitu ambacho pia napenda niseme kidogo, kwamba kuna watu wanakawaida ya kubashiri reversal mahali itakapoenda kufanyika kwakuangalia mikunjo so wengine wanadiriki hata kuweka pending order wakiamini price ikifika hapo ni lazima itageuka tu…utakufa kama unafanya hivi coz forex huwa tunatrade tunachokiona so ukianza kubashiri kwamba price ikifika sehemu Fulani lazima igeuke eti kisa kuna resistance au support kongwe acha, na utakua unakosa fulsa kila siku maana utakaa sana kusubiri na price inaweza isifike hapo so unabaki kushangaa tu.

Wataalamu wanasema ni ngumu kutambua reversal hadi itokee na hata big boys wenyewe hawana uwezo wa kutambua reversal sema wao wananguvu kwenye order so big boy mmoja anaweza akaweka order ya matrader wengi sana na akayumbisha soko mahali anapotaka liende yeye and si kweli kwamba wanaweka pending order kwenye zile zone za zamani let say kwenye zone ambayo ni ya miezi kadhaa ilitokea nyuma, hii ni biashara and watu wa nataka wapate ela kila siku so inaingiaje akilini mtu akaweke pending order kwenye zone itakayofikiwa na price ndani ya mwezi au miezi obvious haiwezekani.

So point muhimu ni kwamba usijiaminishe kubashiri reversal ya price kwenye ukanda wa zamani maana si sahihi ila huwa tunaingia au kubashiri kwenye zone ambayo imefikiwa na hapo ndipo ambapo jicho la matrader wengi duniani linapokua na watu sasa wanaanza kuweka order zao hapo na watakao shinda kuwa na order nyingi basi wanakua wameshinda kuipeleka price kwenye upande wanaoutaka wao.

Hii ni muhimu sana kaa nayo kichwani….

Jinsi ya kutambua hizo zone

  1. Demand na supply huwa sheria yake namba moja tunaangalia uwezo wa price kugonga na kutoka kwenye hiyo zone, kama tulivyosema awali ili zone ya demand au supply iwe valid basi ni lazima iguswe na candle zisizozidi tatu, maana hii ni zone so tunategemea kupata order nyingi kwahiyo wingi wa order utapelekea price isikae sana kwenye hilo eneo na endapo itakaa sana basi hiyo zone ni dhaifu coz inaonekana nguvu ya order zilizowekwa na seller na buyer haina utofauti mkubwa that’s why price haimove katika ubora.
  2. Hakikisha haubashiri zone kwenye eneo ambalo unaamini itaenda kutokea kisa tu hilo eneo ilishawahi tokea zone siku za nyuma, ndio labda unaweza ukajiambia kwamba hapo mahali huwa kuna pending order but kumbuka pending order sio order mbaka iwe order so haina madhara kwenye movement ya price, kwahiyo kuna mawili price ifike hapo ipiyilize au price ifike hapo irudi ilikotoka na au price ifike hapo ikae kwenye hali ya uwiano.
  3. Ukanda mzuri ni ule ambao unatokea mahali ambapo kuna nafasi kubwa nyeupe, yani price haijafika hilo eneo kwa muda mwingi sana, kwasababu lazima itakua ni juu sana au itakua ni chini sana na hakuna trader ambae hapendi kubuy low na kusell high so zone ikitokea maeneo hayo huwa tunasema imetokea mahali ambapo mauzo yalifanyika mengi mno au manunuzi yamefanyika mengi mno kwahiyo reversal itatokea, ila usisahau forex sio science so hii si sheria hadi ikamilike yani hadi itokee.
  4. Hakikisha ukanda wako umeendana sawa na trend ya kwenye D1 hasa kama wewe ni intra day trader, hii itakufanya uwe na uhakika na kuhold kwa siku nzima maana uelekeo wa soko upo sawa na ulipoweka order yako siku hiyo.
  5. Hakikisha hauchukui zone ambayo imetokea katikati mwa price, coz hizi huwa zinakuaga ni trap za market marker, na nnaposema katikati namaanisha kabla trend haijaonesha kubadilika we ukaingia kwenye retracement hapo lazima ufe, kwasababu big boys huwa wanalichukua soko toka mwanzo mwa trend then wanapanda nalo au wanashuka nalo katika sheria zile zile za 3 impulse and 2 correction so watakwenda nalo then watafika mahali watachukua faida zao hapo utaona kama trend ni up basi soko linashuka kidogo na hapa kuna watu wanavutiwa wataingia hasa wale wa like yes yes soko linashuka hili unatia order yako wataacha tuingie kwawingi then wanarudi tena kwenda kukamilisha trend hapo ndio unaanza kulia, kwahiyo usifanye hivo.

Jinsi ya kuchora hizo kanda, na nilazima kabla ya kujua kuchora tujue hizo zones au kanda huwa zinakua zipo katika mafungu mafungu, kwahiyo ukiiona zone ni lazima uelewe hii ni zone ya aina gani.

Ngoja tuongee kuhusu hizi zone zinazosababishwa na big boys pindi wanapochukua faida na zile zinazosababiswa na big boys pindi wanapoweka order.

Kuna wakati unaweza ukafungua Mt4 yako ukakuta trend ni up ila ikawa inaenda juu then inashuka kwa pips kadhaa halafu inarudi tena kuendelea na trend na wakati inashuka huwa inatengeneza zone basi hii ndio huwa tunaita zones ambazo zimesababishwa na hawa jamaa big boys kuchukua faida zao.

Pia kuna zile zone ambazo ukifungua Mt4 yako utazikuta zinaanzia juu kwenye supply au chini kwenye demand na zinakwenda moja kwa moja katika uelekeo wa trend huku ikitengeneza HH,HL na LH,LL ambazo hazifiki kwenye mahali ambapo zone ipo, hii ndio inaitwa zone ambayo imesababishwa na big boys kuweka order na kinachofanya price isifike kwenye mahali ambapo hizi order zipo ni kwamba hawa jamaa big boys huwa hawaruhusu kitendo hiki kitokee coz wanahofia endapo wataruhusu price ifike kwenye usawa wa order zao basi wananweza wakawavutia wawekezaji wengine wakadhani kwamba hii zone sasa imekwisha muda wake so ni muda wa kuweka order nyingi ambazo zikifanikiwa kuwa nyingi kuliko zilizokuwa kwenye hiyo zone basi price itakwenda kinyume na wao na kupelekea wao kupata hasara.

So hii ni muhimu ambayo ni lazima tuifahamu kwamba zone inayosababishwa na big boys wakati wanachukua faida huwa inakwenda na kurudi mahali kwa awali then inavunja hiyo zone na kwenda juu zaidi kama trend ilikua up au kushuka chini zaidi kama trend ilikua down.

Ila zone inayosababishwa na uwepo wa order nyingi za big boys huwa price ikienda chini kwa downtrend itatengeneza hizo swing za LH, LL ambazo haziwezi kufikia mahali ambapo order iliwekwa, kwanini iko hivi? Hii ni kuonesha kwamba zone bado imara.

Jifunze Forex Kiswahili

Ukiangalia hiyo picha hapo juu trend ni down na Mimi nimejaribu kuonesha kwenye upande wa zone za supply tu ila ukiangalia kwa umakini kwa chini ya hizo zone utaona vijizone vidogo vya demand pia, so navo ni muhimu ukiwa unafanya analysis uvichoree, ila hiyo picha hapo inaonesha upande wa supply na kwa jina moja unaweza ukaiita drop base drop, kwamaana inakua inashuka then inatengeneza consolidation kidogo then inashuka tena, so ndio maana ikaitwa drop base drop…coz inaanza kushuka inatengeneza base ambayo ndio consolidation halafu inakuja kushuka tena…tutaiongelea baadae hii drop base drop, rally base rally na drop base rally pamoja na rally base drop.

Jifunze Forex Kiswahili

Hii ni ile aina ya zone ambayo inatokea baada ya big boys kuchukua faida, iangalie vizuri hapo

Ukirejea hapo nyuma nliwahi kusema uimara wa zone haupimwi na ukongwe wake ispokua zone inatokea pale tu ambako kuna uwingi wa order, ila kuna wakati ukijaribu kuangalia unaweza ukaona zone ambayo ilitokea mwezi uliopita katika D1 ukaona na leo imefikiwa tena na price na inafanya reversal hapo, hapa wengi watapingana na hiyo kauli kwamba zone haipimwi kwa ukongwe wake….ila hiyo kauli iko sahihi ispokua price ikitoka kwenye zone wanasema inaweza ikarudi baada ya muda flani na hii ni kulingana na timeframe ambayo wewe unatumia, kwamfano kwenye 1H timeframe price ikitoka kwenye zone na ikarudi baada ya 24hours basi hii zone tunasema bado iko valid ila ikichelewa kurudi basi hii zone tunasema haiko valid.

Pia kwenye D1 timeframe price ikitoka kwenye zone ili hiyo zone iendelee kuwa valid basi lazima ije irudi baada ya siku 30 kinyume chake basi hiyo zone haitokua valid tena, so ndio maana kuna wakati unaweza ukaona zone ambayo unaamini ni kongwe lakini bado ikawa iko valid ni kutokana na kwamba price ilirudi kwenye eneo hilo kwa muda sahihi na sio kwamba eti ni kongwe hapana.

Sasa unaweza ukajiuliza kwanini price ikitoka kwenye zone itaenda then itarudi baada ya muda flani?

Hii inatokana na kwamba, banks nyingi huwa zinapenda kuweka order zao kwenye zone so price ikifika kwenye zone tu basi bank wataweka order zao hapo, kama ni kwenye supply basi wataweka order za kusell na kama ni kwenye demand basi wataweka order za kubuy, sasa kipindi wanapobuy au kusell katika zone watakwenda na price katika umbali ambao wao watahitaji then wakishafika hapo basi wataanza kuchukua faida zao na kipindi wanafanya hivi basi reversal itatokea na price itaanza kugeuka kurudi tena kwenye zone, na hapa sasa watawavutia ma retailer wengi watadhani sasa trend imechange wataanza kuingia na price ikifika tena kwenye zone bank watatumia ile faida yao waliyoipata kurudisha tena price kule ilikotoka na hapa wengi wataliwa ela zao….hii ni sababu ya kwanza.

Sababu ya pili ni kwamba bank nyingi huwa hazipendi kuuza au kununua katika umbali ambao price zimeachana sana, so ili iwe rahisi kwa wao kucalculate faida wanayohitaji basi wataweka order kwenye zone wataishusha price ila katika izo order kuna zingine zitasalia kwenye zone so watakwenda na order chache then wakishapata faida wanayoitaka watamanipulate soko yani watalipeleka vile wao wanataka na hapa watachukua faida then price itarudi kule kwenye order zao then wataziingiza na hizo order sokoni tena na hapo mambo yatarudi yalikotoka so hii pia itawasababishia watu wengi yani akina sisi kula za us

Ila kuna wakati unaweza ukaona price imetoka kwenye zone ikaenda kwenye upande tarajiwa kwenye upande wa supply au upande wa demand, ila baadae ikafika sehemu price ikawa inarudi sasa ilikotoka na ikafika kwenye zone ikapitiliza hadi upande wa pili, hapa tunasema hao mabank hapa walishatoka so hakuna order ambazo zilibaki kwenye hiyo zone na ndio maana price iliporudi kwa Mara ya pili ikapitiliza, na hapa sasa investor wengine wataingia coz wataamini zone ambayo ilikuepo mwanzo now imekua si valid tena kwahiyo nao wataweka order zao then price itakwenda kwenye upande ambao order ni nyingi.

NB:
Wingi wa order hausababishwi na uwingi wa watu katika demand au katika supply, isipokua anaweza akawa mtu mmoja tu ambae anaela nzuri akaweka order za kutosha na akayumbisha soko na hata kama upande mwingine unawatu elfu kumi ila wakawa na order ambazo ndogo kuliko alizotoa huyo mtu mmoja basi hawatokua na ujanja wa kuyumbisha soko richa ya uwingi wao…na hii aliifanya George Soro

You may also like...

Leave a Reply